WACHEZAJI WA ZANZIBAR HEROES WAINGIA KAMBINI, WAPANGIWA BONGE LA HOTELI


Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar heroes kinachojiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenji CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba 3-17, 2017 nchini Kenya leo kimeingia Kambini kwenye Hoteli ya Zanzibar Paradise International Hotel iliyopo Amaan, huku nyota wengine wanaocheza ligi kuu soka Tanzania bara wakitarajiwa kuwasili kuanzia Jumatatu.

Kwenye Mashindano ya CECAFA Zanzibar wapo Kundi A ambalo lina timu ya Taifa ya Zanzibar, Tanzania Bara, Libya, Rwanda na wenyeji Kenya huku Kundi B kuna Mataifa ya Sudan ya Kusini, Ethiopia, Zimbabwe, Burundi na Uganda.

Wachezaji waliyoanza mazoezi ni Walinda mlango Ahmed Ali "Salula" (Taifa ya Jang'ombe) na Mohammed Abdulrahman "Wawesha" (JKU), Nassor Mrisho (Okapi), Walinzi Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed "Sangula"(Jang'ombe Boys), Abubakar Ame "Luiz" (Mlandege), Issa Haidar "Mwalala" (JKU) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang'ombe).

Viungo Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang'ombe), Amour Suleiman "Pwina" (JKU), Hamad Mshamata (Chuoni), Omar Juma "Zimbwe" (Chipukizi) na Mbarouk Marshed (Super Falcon), Suleiman Kassim "Seleembe" (Majimaji), Mohammed Issa "Banka" (Mtibwa Sugar) pamoja na washambuliaji Ali Badru (Taifa ya Jang'ombe), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa "Rais" (Jang'ombe boys), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto) pamoja na Mwalimu Mohd (Jamhuri).

Wachezaji ambao wanatokea ligi kuu soka Tanzania bara ambao bado hawajajumuika na wenzao ni Walinzi Abdallah Haji "Ninja" (Yanga), Adeyum Saleh "Machupa" (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abdulla Kheir "Sebo" (Azam), Viungo Mudathir Yahya (Singida United), Matteo Anton (Yanga), Seif Rashid Abdallah “Karihe” (Lipuli) na Kassim Suleiman (Prisons) .

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA