ZANZIBAR HEROES YAAGWA, WAAHIDI KUBEBA KOMBE LA CHALENJ
Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) imeagwa rasmi leo na kukubidhiwa bendera ya Taifa, wimbo wa Taifa
pamoja na jezi za Taifa na tayari kwaajili ya kuiwakilisha nchi katika
Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kuanza rasmi Disemba
3-17, 2017 nchini Kenya.
Timu hiyo yenye
jumla ya wachezaji 24 imekabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari Utalii
Utamaduni na Michezo, Rashid Ali Juma.
Akizungumza na
Waandishi wa habari Waziri Rashid amesema Wizara yake iko bega kwa bega na
wadau wa michezo katika kuhakikisha kuwa sekta hiyo inapiga hatua.
Kwa upande wake
Kocha mkuu wa Zanzibar Heroes Hemed Suleiman (Moroco) amesema yeye ni mzowefu
katika Mashindano hayo huku akiwatoa wasi wasi Wazanzibar kwa kusema kuwa
vijana wake watafanya vyema katika Mashindano hayo.
Mara baada ya
kupokea bendera ya Taifa Nahodha wa timu hiyo Suleiman Kassim “Seleembe”
amesema kuwa wao wamejiandaa kikamilivu na wanajua wanabeba dhamana kubwa kwa
Wazanzibar wote, hivyo watahakikisha wanapambana na kubeba ubingwa.
Comments
Post a Comment