LARSON WA MAFUNZO APIGA BONGE LA BAO WALIPOICHAPA POLISI
Ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja imeendelea tena jioni ya leo kwa kupigwa mchezo mmoja katika Uwanja wa Amaan ambapo timu ya Mafunzo Wazee wa Jela jela wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu baada ya kuichapa Polisi bao 1-0.
Bao pekee la Mafunzo limefungwa na Ali Juma (Larson) dakika ya 5 ya mchezo huo baada ya kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Polisi Said.
Ligi kuu soka ya Zanzibar kesho itasimama na kupisha ligi daraja la kwanza Taifa Unguja ambapo katika uwanja wa Amaan kesho Villa United watakipiga na Mundu, katika uwanja wa Mwanakombo Kijichi watasukumana na Ngome huku katika uwanja Bungi Stronge Fire watacheza na Mlandege michezo yote itapigwa majira ya saa 10:00 za jioni.
Comments
Post a Comment