MABINGWA ZU WATUA NYUMBANI NA KUPATA BONGE LA MAPOKEZI
Mabingwa wa Mashindano ya Vyuo Vikuu Tanzania maarufu TUSA, Chuo
cha Zanzibar University (ZU) wamerejea nyumbani Zanzibar na kupokelewa kwa shangwe
na wanafunzi wenzao pamoja na wapenzi wa soka wa Zanzibar.
ZU wamerejea wakitokea
Mjini Dodoma siku chache baada ya kubeba ubingwa huo kwa kushinda 4-0 dhidi ya
wapinzani wao Chuo cha St John cha Dodoma.
Comments
Post a Comment