MWENGE NA MLANDEGE ZAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI, BADAE TAIFA NA ZIMAMOTO

Timu ya Mwenge na Mlandege zimeanza vyema Mashindano ya Kombe la Mapinduzi kwenye michezo iliopigwa leo kwenye uwanja wa Amaan.

Mlandege waliwachapa JKU mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa saa 8 za mchana ambapo mabao ya Mlandege yamefungwa na Khamis Abuu dakika ya 18 na Abubakar Ame (Luiz) dakika ya 60 huku bao pekee la JKU limefungwa na Khamis Abdallah katika dakika ya 34.

Nao Mwenge wamefanikiwa kuwachapa bao 1-0 timu ya Jamhuri kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo huku bao pekee la Mwenge likifungwa na Ali Salim Bajaka dakika ya 31 ya mchezo.

Badae saa 2:15 usiku utapigwa mchezo mwengine kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya Zimamoto kwenye uwanja wa Amaan.

Mashindano hayo yataendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 10:00 za jioni Zimamoto  watakuwa na kazi ngumu kucheza JKU na Saa 2:15 Taifa ya Jan’gombe watakipiga na Mlandege.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA