ZANZIBAR HEROES HAO KISIWANI PEMBA KUFUNGA MWAKA 2017 KWA FURAHA


Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kesho saa 1 asubuhi watasafiri kwa Boti kwenda Kisiwani Pemba na huko watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Kombaini ya Pemba.

Mechi hiyo itachezwa kesho kutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Gombani mjini Pemba.

Safari hiyo ya kwenda Pemba ilipendekezwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kwenye tafrija maalum iliyoendana na Taarab ya kikundi cha Taifa cha Zanzibar ambapo siku hiyo pia Rais huyo aliwazawadia Wachezaji na Viongozi Milioni 3 na kiwanja kila mmoja.

Zanzibar Heroes imefanikiwa kushika nafasi ya pili ya michuano hiyo ya ‘CECAFA’ baada ya kupata matokeo ya kufungwa magoli 3-2 kwa changamoto ya mikwaju ya penanti baada ya kwenda sare ya goli 2-2 kwa dakika 120 na timu ya Taifa ya Kenya.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA