ZANZIBAR HEROES YABANWA NA KOMBAIN YA PEMBA, SASA WAPO KWENYE TAARABU KULA BATA


NA JUMA MUSSA – ZBC PEMBA

Washindi wa pili wa michuano ya CECAFA CHALLENGE CUP 2017 timu ya Zanzibar Heroes imewasili kisiwani Pemba kwa ajili ya kukamilisha sherehe yao na kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Pemba Kombaini ikiwa ni miongoni mwa ahadi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi mh dokta Ali Moh’d Shein ya kukipeleka kikosi hicho kisiwani Pemba kutoa burudani kwa wakaazi wa huko.

Kwenye mapokezi hayo yaliyoongozwa na Naibu Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo mh Choum Khamis Kombo na wapenda michezo ,  Waziri huyo amewataka wananchi kuwapa hamasa wachezaji hao ili kuweza kufanya vyema katika michezo mingine itakayoshiriki.

Ikicheza mbele ya mashabiki walijitokeza kuisapoti timu hiyo katika uwanja wa Gombani Zanzibar Heroes ilishuhudiwa wakishidwa kuwaumiza mashabiki wa Pemba Kombaini baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana.

Hata hivyo the Heroes itabidi kujilaumu wenyewe baada ya kukosa mabao mengi kwa kushindwa kuzitumia vyema nafasi walizozipata ambapo mashuti yao yaliishia kutoka nje au kugonga mtambaa panya.

Katika hatua nyingine timu hiyo ya Zanzibar Heroes usiku huu itakuwepo tena Gombani kuhudhuria  burudani ya taarabu kutoka kikundi cha taifa pamja na mashabiki wa Pemba .

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA