ZANZIBAR YATINGA FAINALI MASHINDANO YA BEACH SOKA, YAONGOZA KULIKO NCHI ZOTE WATACHEZA TENA NA MALAWI FAINALI
Timu ya taifa ya Zanzibar ya soka la ufukweni (Zanzibar Sand
Heroes) imefanikiwa kutinga fainali katika Mashindano ya Copa Dar es salam
yanayoendelea katika Ufukwe wa Coco Jijini Dar es salam baada ya asubuhi ya leo
kuwachapa Malawi mabao 5-1.
Mchezo mwengine leo Uganda wakaichapa Tanzania bara kwa mabao
6-5.
Kwa matokeo hayo Zanzibar imeongoza katika Mashindano hayo
wakishika nafasi ya kwanza huku Malawi wamekamata nafasi ya Pili ambapo
Tanzania bara wakishika nafasi ya tatu na Uganda wakikamata nafasi ya nne.
Hivyo fainali itachezwa na timu ilokamata nafasi ya kwanza
(Zanzibar) dhidi ya timu iloshika nafasi ya pili (Malawi) huku mshindi wa tatu
watachuana kati ya timu iloshika nafasi ya tatu (Tanzania Bara) na Uganda
waliomalizia nafasi ya nne.
Michezo hiyo itapigwa jioni ya leo Jumanne katika fukwe za
Coco ambapo utaanza kuchezwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kisha kumalizwa
fainali.
Comments
Post a Comment