KESHO FAINALI MBILI ZA MAPINDUZI CUP KUPIGWA KATIKA UWANJA WA AMAAN
Fainali ya 12 ya michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup inatarajiwa
kupigwa kesho kwenye dimba la Amaan kati ya mabingwa watetezi Azam fc kutoka
Tanzania bara dhidi ya URA kutokea Uganda, mchezo ambao utapigwa majira ya saa
2:15 za usiku.
Bingwa wa Mashindano hayo atazawadiwa Kombe,
Shilingi Milioni 10 na Medali za dhahabu wakati mshindi wa pili atapata Milioni
5 na medali za fedha.
Wakati huo huo pia kesho kutachezwa Fainali ya
ZBC watoto mapinduzi cup mchezo utapigwa majira ya saa 10:30 za jioni kati
ya Wilaya ya Mjini dhidi ya Mkoani katika uwanja wa Amaan.
Mapema kesho saa
8:00 za mchana uwanjani hapo utachezwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya
Wilaya ya Chake cheke dhidi ya Wilaya ya Kati.
Bingwa wa
Mashindano hayo atazawadiwa Fedha Taslim shilingi milioni 1, seti moja ya jezi,
Kombe kubwa na Medali za dhahabu wakati mshindi wa pili atazawadiwa shilingi
laki 7, seti moja ya jezi, kombe na medali za fedha huku mshindi wa tatu
atapata shilingi laki 3, kombe dogo, seti moja ya jezi na medali ya shaba.
Comments
Post a Comment