MZEE ZAM WA ZANZIBAR APEWA FUPA NA CAF
Shirikisho la Soka
Barani Afrika (CAF), limemteua Mzee Zam Ali kutoka Zanzibar kuwa Kamishna wa
mchezo nambari 50 wa kombe la shirikisho kati ya FC Platinum ya Zimbabwe dhidi
ya Club Desportivo 1 de Agosto ya Angola mchezo utakaopigwa 20 au 21 ya
February, 2018 huko Zimbabwe.
Mzee Zam
atawasimamia Waamuzi wa Afrika ya Kusini watakaochezesha mchezo huo akiwemo
muamuzi wa kati Christopher Harrison, akisaidiwa na muamuzi namba moja Sandile
Dilikane na muamuzi namba mbili Thembisile Theophilus huku Muamuzi wa akiba
akiwa Tinyiko Victor Hlungwani.
“Nimefurahi CAF
kuendelea kuwa na imani na mimi kwani wananijua vyema hasa hivi karibuni
nilikuwa Kamishna katika Mashindano ya CECAFA Senior Challenge Cup yaliofanyika
nchini Kenya, mimi ni mzoefu kuchaguliwa kwenye shughuli za soka kama hizi
katika Mashindano mbali mbali”. Alisema Mzee Zam.
Comments
Post a Comment