SIMBA YAAGA RASMI KOMBE LA MAPINDUZI, SASA YAUNGANA NA TIMU 6 ZA ZANZIBAR KWENDELEA NA KAZI NYENGINE
Timu ya Simba Sports Club imetolewa rasmi katika Mashindano
ya Kombe la Mapinduzi baada ya jioni ya leo kufungwa bao 1-0 na URA kwenye
mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Amaan.
Mchezo huo ulikuwa na kasi huku Simba ikihitaji ushindi ili
iingie nusu fainali wakati URA walihitaji japo sare ambapo mpaka dakika 90
kumalizika Simba akikubali kulala mbele ya Waganda hao wa URA.
Bao pekee la URA limefungwa na Kalama Deboss dakika 45.
Mara baada ya kumalizika mchezo huo kocha wa Simba Masoud
Djuma amekiri kuwa Mashindano magumu lakini wamejifunza mengi licha ya kutolewa
na sasa wanajiandaa kufanya vyema kwenye ligi kuu soka Tanzania bara.
Nae Paulo Okata kocha wa URA amesema sasa kikosi chake
kinazidi kuimarika kila siku huku akiwa hana wasi wasi kukutana na timu yoyote
kwwenye nusu fainali kati ya Singida United au Yanga.
Katika Kundi hilo A timu URA imeongoza ikimaliza na alama 10,
huku Azam ikishika nafasi ya pili kwa points zake 9 na sasa URA anasubiri
mshindi wa pili wa kundi B kati ya Yanga au Singida United ambao kwasasa
wanacheza kwenye mchezo wa mwisho wa kundi B ambapo Yanga ana alama 12 sawa
sawa na Singida ambao wote wameshatinga nusu fainali kwenye kundi lao B.
Sasa Simba wataungana na timu sita za Zanzibar ambazo
zimeshatoka zikiwemo JKU, Zimamoto, Taifa ya Jang’ombe, Mlandege, Mwenge na
Jamhuri.
Baadhi ya Waamuzi wanaochezesha kombe la Mapinduzi wakitokea Zanzibar |
Comments
Post a Comment