DIAMOND AANZA KUSAKA WATANGAZAJI WA WASAFI RADIO NA TV, WAZIRI WA MICHEZO ZANZIBAR AWAOMBA WAZANZIBAR WAJITOKEZE KWA WINGI NGOME KONGWE KESHO
Waziri wa Habari Utalii Utamaduni
na Michezo Rashid Ali Juma amewataka watangazaji pamoja na watu wenye vipaji hivyo
kujitokeza kwa wingi katika zoezi maalum la kutafuta vipaji hivyo zoezi ambalo
litafanyika kesho Jumanne kuanzia saa 3 asubuhi hadi jioni katika ukumbi wa
Ngome Kongwe.
Waziri Rashid ameyasema hayo Afisini
kwake Kikwajuni wakati akimkabidhi msanii Nasib Abdul maarufu Diamond hati ya
leseni ya kufungua vituo vya wasafi Radio na TV.
Kwa upande wake Diamond amesema
ameamua kufika Zanzibar kutafuta vipaji hivyo kwani anajua Zanzibar kuna vipaji
vingi huku akiwataka Wazanzibar wajitokeze kwa wingi katika zoezi hilo ili
wapate fursa ya ajira.
Comments
Post a Comment