JKU APIGWA 7-0 KOMBE LA KLABU BINGWA HUKU ZIMAMOTO AKIFA KIUME KOMBE LA SHIRIKISHO
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya klabu Bingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika JKU na Zimamoto zote zimetolewa rasmi leo katika Mashindano hayo baada ya kufungwa ugenini katika michezo yake ya marejeano.
Katika kombe la Klabu Bingwa JKU wamefungwa na Wenyeji Zesco
ya Zambia mabao 7-0 na kufanya kutelewa kwa jumla ya mabao 7-0 kufuatia mchezo
wa awali uliochezwa Amaan Zanzibar kumalizika kwa sare ya 0-0.
Mabao ya Zesco manne yamefungwa na Zikiru Adams dakika 4, 42, 57, 60 huku
mengine yakifungwa na Lazarus Kambole dakika 36, Winston Kalengo dakika 77 na
Lameck Banda dakika ya 87.
Kwa upande wa Zimamoto ambao walikuwa wanawakilisha Zanzibar
katika Kombe la Shirikisho nao wametolewa kwa kufungwa 1-0 na wenyeji wao
Wallaita Dicha ya Ethiopia na kufanya watolewe kwa jumla ya mabao 2-1.
Bao pekee la Wallaita Dicha limefungwa na Arafat Djako dakika
ya 29.
Huu ni mfululizo wa kufanya vibaya kwa vilabu vya Zanzibar
katika Mashindano hayo kufuatia msimu uliopita timu ya Zimamoto
na KVZ zilitolewa katika hatua ya awali kwenye Mashindano hayo .
Kwenye klabu bingwa Zimamoto ilitolewa na timu ya Ferroviario Beira ya
Msumbiji baada ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa mwisho wa ugenini ambapo
awali nyumbani walishinda 2-1 hivyo wakatolewa kwa kufungwa jumla ya mabao 4-3.
Na kombe la Shirikisho timu ya KVZ nayo ilitolewa katika mashindano hayo
baada ya kufungwa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Messager Ngozi ya Burundi baada ya
mchezo wa mwanzo uliochezwa Zanzibar KVZ walishinda 2-1, hivyo walitolewa kwa
kufungwa jumla ya mabao 4-2.
Wachezaji wa JKU kushoto Amour Suleiman (Pwina) na kulia Issa Haidar (Mwalala) |
Comments
Post a Comment