JKU WABANWA MBAVU NYUMBANI KWAO NA ZESCO YA ZAMBIA
Wawakilishi
wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Afrika timu ya JKU imelazimishwa
sare ya 0-0 nyumbani kwao kwenye uwanja wa Amaan dhidi ya Zesco United kutoka
Zambia.
Katika mchezo huo ambao
ulikuwa na ushindani wa hali ya juu na mashambulizi yakushutukizia dakika
tisini za muamuzi JeanClaude Ishimwe kutoka Rwanda hakuna timu iliyoona lango
la mweziwe zaidi ya kosa kosa nyingi kwa kila timu.
Akizungumzia mchezo huo
kocha wa timu ya JKU Ali Suleiman Mtuli amesema mchezo ulikuwa nzuri na
wanajipanga kwa ajili ya mchezo ujao utakaochezwa huko Zambia.
Nae Haji Juma (Chafu)
mlinda mlango wa JKU amefanikiwa kuwa nyota wa mchezo huo na amesema
wataendelea kupigana ili waiwakilishe vyema Zanzibar katika Mashindano hayo.
Nae kocha wa timu ya
ZESCO United Tenant Chembo amesema
ameyapokea matokeo hayo huku wakijipanga kwa mchezo wao wa marejeano nyumbani
kwao.
Wawakilishi
wengine wa Zanzibar timu ya Zimamoto watarajiwa kujitupa dimbani kesho mnamo
majira ya saa kumi alsiri kukipiga na timu ya Wolaitta Dicha kutoka nchini
Ethiopia ikiwa ni mchezo wa kwanza wa kombe la shirikisho barani Afrika.
Comments
Post a Comment