MASHINDANO YA HALF MARATHON YAFANA ZANZIBAR
Mashindano ya Zanzibar Half Marathon yenye lengo la
kuibua vipaji kwa vijana, kuviendeleza na kuwandaa vijana hao katika mashindano
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yamefanyika hii leo Foradhan Mjini Unguja huku
washiriki zaidi ya 500 kutoka nchi mbali mbali walishiriki Mashindano hayo kwa
kilomita 5, 10 na 21.
Akizungumzia Mashindano hayo Mwenyekiti wa
Chama cha Riadha Zanzibar Abdul Hakim Cosmas Chasama amesema Mashindano hayo
yamewapa mazoezi mazuri wanaridha ambao watashiriki Mashindano mbali mbali
makubwa yakiwemo ya ndani na nje ya Tanzania.
Mshindi wa kwanza Kilomita 21 Wanaume
amefanikiwa kuwa Dickson Marwa kutoka Tanzania Bara huku nafasi ya pili
ikichukuliwa na Mohammed Ramadhan Mgeni kutoka Zanzibar huku nafasi ya tatu
ikikamatwa na Remigius John kutoka Tanzania bara.
Kwa upande wa Wanawake Kilomita 21 Mshindi ni Angel
John Juma kutoka Tanzania bara huku nafasi ya pili ikikamatwa na Asma Rajab kutoka
Zanzibar wakati nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mia Vejlgaard Just kutoka
Denmark.
Na katika kilomita 10 Wanaume mshindi ni Abdallah
Jecha Abdallah kutoka Zanzibar, mshindi wa pili ni Filipo Jacob Mambo kutoka
Tanzania bara huku Said Khamis Ali kutoka Zanzibar akishinda nafasi ya tatu.
Kwa upande wa Wanawake kilomita 10 washindi ni
Rosemery Gustaph Malki kutoka Zanzibar huku nafsi ya pili ikikamatwa na
Warda Shaaban Mbura kutoka Zanzibar na nafasi ya tatu ikichukuliwa na Maria Michael
Benedictor kutoka Tanzania bara.
Comments
Post a Comment