ZANZIBAR HEROES MAPEMA KUTANGAZWA NA KUANZA MAANDALIZI
Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo imesema itahakikisha
Chama cha soka Zanzibar (ZFA) inasimamia kufanya maandalizi ya timu ya taifa ya
Zanzibar (Zanzibar Heroes) mapema mwaka huu ili izidi kutoa upinzani mkali
katika mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup.
Akijibu swali lililoulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Konde
Omar Seif Abeid aliyetaka kujua wizara ina mpango gani kabambe uliondaliwa
kuhakikisha Zanzibar Heroes inaendelea kutoa upinzani katika mashindano hayo,
naibu waziri wa wizara hiyo Chum Kombo Khamis amesema wizara kwa kushirikiana
na idara ya michezo itahakikisha kuwa ZFA inasimamia kufanyika maandalizi ya
timu hiyo mapema ili kuleta ushindani katika mashindano hayo.
Zanzibar Heroes ilifanikiwa kushika
nafasi ya pili katika mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup mwaka jana baada
ya kufungwa kwa penalty 3-2 na wenyeji Kenya kufuatia kutoka sare ya 2-2 ndani
ya dakika 120.
Comments
Post a Comment