ZANZIBAR HEROES WAKABIDHIWA VIWANJA VYA PLAN HUKO TUNGUU
Wachezaji na
Viongozi 33 wa Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)
wamekabidhiwa hati zao za viwanja walivyoahidiwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein aliyoitoa Disemba 23,
2017.
Wakikabidhiwa
Viwanja hivyo eneo la Tunguu Plan na Waziri wa ardhi, maji, nishati na
mazingira Salama Aboud Talib amewataka kuvienzi na kuvitunza kama walivyoagizwa
na Dkt Shein kuwa wasiviuze bali wavitumie katika kujenga maisha yao.
Amesema
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini Michezo ndio maana ikawazawadia
viwanja pamoja na zawadi mbali mbali.
Nae waziri wa habari utalii utamaduni na michezo
Rashid Ali Juma amesema leo ni siku ya historia kwa mashujaa hao baada ya
kukabidhiwa rasmi viwanja vyao walivyoahidiwa na rais wa zanzibar na kuwahimiza
kuendelea kujituma kwani michezo ni ajira.
Kwa upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Hemed Suleiman
(Morocco) amemshukuru Dkt Shein kwa ahadi yake kutimizwa leo huku wakiwa nafura
kubwa sana kwa tukio hilo.
Wachezaji wa timu hiyo wamefurahishwa baada ya rais wa
Zanzibar kutimiza ahadi yake ya kuwapatia na kumpongeza kwa juhudi zake za
kupenda na kuthamini michezo.
Zanzibar
Heroes ilifanikiwa kushika nafasi ya pili katika Mashindano ya Cecafa Senior
Chalenj Cup Mwaka jana baada ya kufungwa kwa penalty 3-2 na wenyeji Kenya baada
ya kutoka sare ya 2-2 ndani ya dakika 120.
Mlinda mlango Ahmed Salula akikabidhiwa hati ya kiwanja na waziri wa ardhi, nishati na mazingira Salama Aboud Talib |
Comments
Post a Comment