ZESCO WAFANYA MAZOEZI KWA SIRI, WATU WOTE WAMEZUILIWA KUINGIA UWANJA WA AMAAN
Timu ya Zesco United kutoka Zambia imezuia mashabiki kuingia uwanja wa Amaan, kuangalia mazoezi ya
klabu hiyo baada ya kuamua kufanya mazoezi siri kuelekea mchezo wao kesho kutwa
(Jumamosi) dhidi ya wenyeji wao JKU katika Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa
Barani Afrika.
Mashabiki wa soka visiwani Zanzibar walijitokeza kwa wingi nje
ya uwanja wa Amaan wakisubiri timu ya ZESCO ifike uwanjani ili waangalie
mazoezi yao, lakini hali ilikuwa tofauti baada ya wachezaji kuingia ndani ya
uwanja huo na Mageti yote yakafungwa na hakuruhusiwa mtu yeyote kuingia.
Kabla ya dakika 15 kumaliza mazoezi wakawaruhusu waandishi wa
Habari tu pekee yao kwaajili ya kufanya mahojiano na kupiga picha.
Hii ni kawaida hasa katika Mashindano kama haya kwa timu kuzuia
mashabiki kwani huwa na wasi wasi kuibiwa baadhi ya mbinu zao pamoja na
kujulikanwa kwa haraka wachezaji wao nyota ambao wanaimani waje kuwafunga
wenyeji wao.
“ Haturuhusu kuingia uwanjani nyinyi muje Jumamosi kuangalia
mechi tu“. Alisema Afisa mmoja wa Zesco.
Mchezo huo utapigwa Jumamosi saa 10:00 za jioni katika uwanja wa
Amaan ambapo siku ya Jumapili muda huo huo kiwanjani hapo watacheza Zimamoto
dhidi ya Walaitta Dicha ya
Ethiopia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.
Comments
Post a Comment