Posts
Showing posts from March, 2018
LIGI KUU ZANZIBAR KANDA YA UNGUJA SI MCHEZO MSIMU HUU, ANGALIA MSIMAMO TIMU 6 ZA MWISHO ZITASHUKA DARAJA
- Get link
- X
- Other Apps
WAZIRI MWAKYEMBE AMJULIA HALI RAIS WA ZAMANI WA ZFA
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe amemjulia hali Rais wa zamani wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) Ali Ferej Tamim nyumbani kwake Shangani Mjini Unguja ambae anasumbuliwa na Uti wa Mgongo. Mwakyembe ambaye ameongozana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo, Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai Mohammed Said. Mwakyembe amesema ameona haya ya kumtembelea mwana michezo huyo kutokana na kazi kubwa aloifanya katika taifa la Tanzania. Nae Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) amesema kutokana na kuongoza vyema ZFA pamoja na kuitangaza Zanzibar kimataifa wameona haja ya kumtembelea. Kwa upande wake Rais wa zamani wa ZFA Ali Ferej Tamim amewashukuru na kuwapongeza viongozi hao kwenda kumjulia hali huku akisema kwasasa amepata afadhali na kuendelea kufata ushauri wa Daktari. Mapema ...
MBIO ZA KUPANDA LIGI KUU ZANZIBAR NYEPESI KWA MLANDEGE, KAZI KWA VILLA, MALINDI NA KIZIMKAZI
- Get link
- X
- Other Apps
UWANJA WA MAO TAYARI USHAANZA KUWEKWA NYASI BANDIA, SASA NI FURSA NYENGINE KWA WAZANZIBAR
- Get link
- X
- Other Apps
Harakati za Ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung uliopo Mpirani Kikwajuni Mjini Zanzibar zinaendelea chini ya Wahandisi wa Kampuni ya Kimataifa ya Zhengtai Group ya Jamhuri ya Watu wa China na sasa wanaendelea na zoezi la uwekaji wa nyasi bandia katika uwanja wa Soka. Mtandao huu imeshuhuidia maendeleo ya uwanja huo yanavyoendelea ambapo kwasasa mafundi hao wanatandaza nyasi bandia huku zoezi hilo likitarajiwa kukamilika muda mchache. Tayari uwanja huo umeshawekwa Taa ambazo zitasaidia kuchezwa michezo hadi usiku huku baadhi ya vifaa vyengine vinazidi kutoa sura mpya ya kukamilika kwa ujenzi huo kadri ya siku zinavyokwenda. Ujenzi wa uwanja huo unafuatia msaada mkubwa ulioidhinishwa na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika azma ya kuimarisha uhusiano wa muda mrefu wa pande hizo mbili ukizingatia heshima uliopewa Uwanja huo wa kuitwa jina la Muasisi wa Taifa la China Hayati Mao Tse Tung. Uwanja huo utakuwa na ...
MUAMUZI MFAUME APIGWA STOP NA ZFA KUPISHA UCHUNGUZI WA CAF
- Get link
- X
- Other Apps
Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimemsimamisha kazi Muamuzi Mfaume Ali Nassor kwa muda mpaka pale Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) watakapotoa taarifa za uchunguzi unaendelea dhidi ya Waamuzi wanne wa Tanzania ambao wanatuhumiwa kupokea rushwa. Mfaume Ali Nassor ni miongozi mwa Waamuzi wa Tanzania waliochezesha mchezo namba 54 wa ligi ya mabingwa barani Afrika kati ya LLB ACADEMIC ya Burundi dhidi ya RAYON SPORTS ya Rwanda ambao kwasasa wako hatarini kufungiwa na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) kama watakutwa na hatia ya upangaji wa matokeo katika mchezo uliomalizika kwa RAYON SPORTS kushinda kwa 1-0 ugenini na kufuzu katika hatua nyengine. Hivi karibuni Shirikisho la Soka Tanzania TFF kupitia Kaimu Katibu Mkuu wake Wilfred Kidao limethibitisha kupokea barua kutoka CAF kufanyiwa uchunguzi waamuzi hao. Kidao alisema kama waamuzi hao wakipatikana na hatia, waadhibiwe ipasavyo na kama wakiwa hawana hatia waachiwe huru. Waamuzi hao ni Mfaume Ali Nasoro amb...
WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.
- Get link
- X
- Other Apps
K ocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza kikosi cha wachezaji 23 ambao wataingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya DR Congo na Algeria. Wachezaji wa tano wa Zanzibar ni mlinda mlango Abdulrahman Mohamed wa JKU, pamoja na viungo Mudathir Yahaya wa Singida United, Feisal Salum wa JKU, Abdulaziz Makame wa Taifa ya Jang’ombe na Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar. Kikosi kamili kilichotangazwa na Mayanga kinajumuisha wachezaji wafuatao: Magolikipa ni Aishi Manula, Abdulrahman Mohamed na Ramadhani Kabwili. Walinzi: Shomari Kapombe, Hassan Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni na Abdi Banda. Viungo: Hamisi Abdallah, Mudathir Yahaya, Said Ndemla, Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Mohamed Issa, Thomas Ulimwengu, Farid Mussa, Shiza Kichuya, Ibrahim Ajib. Washambuliaji: Mbwana Samatta, John Bocco, Simon Msuva na Yahaya Zayd. Mara ya mwisho Mayanga alitaja kikosi cha Stars Oktoba 24,...