WAZIRI MWAKYEMBE AMJULIA HALI RAIS WA ZAMANI WA ZFA
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania Dkt
Harrison Mwakyembe amemjulia hali Rais wa zamani wa Chama cha Soka Zanzibar
(ZFA) Ali Ferej Tamim nyumbani kwake Shangani Mjini Unguja ambae anasumbuliwa
na Uti wa Mgongo.
Mwakyembe ambaye ameongozana na Waziri wa Habari, Utalii na
Mambo ya kale Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo, Katibu wa Wizara ya Vijana,
Utamaduni, Sana na Michezo Omar Hassan (King) na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Simai
Mohammed Said.
Mwakyembe amesema ameona haya ya kumtembelea mwana michezo
huyo kutokana na kazi kubwa aloifanya katika taifa la Tanzania.
Nae Katibu wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sana na Michezo Omar
Hassan (King) amesema kutokana na kuongoza vyema ZFA pamoja na kuitangaza Zanzibar
kimataifa wameona haja ya kumtembelea.
Kwa upande wake Rais wa zamani wa ZFA Ali Ferej Tamim
amewashukuru na kuwapongeza viongozi hao kwenda kumjulia hali huku akisema
kwasasa amepata afadhali na kuendelea kufata ushauri wa Daktari.
Mapema leo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Tanzania
Dkt Harrison Mwakyembe amekutana na Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya kale
Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni,
Sana na Michezo Ali Karume kwa lengo la kujuwana na kupanga mikakati yao
ikiwemo masuala ya michezo yanayogusa pande zote mbili za Muungano wa Tanzania.
Comments
Post a Comment