KARUME BOYS WAKABIDHIWA BENDERA, TAYARI WAMESHAPANDA PIPA KWENDA BURUNDI KATIKA MASHINDANO YA CECAFA
Naibu Waziri wa Vijana
Utamaduni Sanaa na Michezo Lulu Msham amekabidhi bendera kwa timu ya taifa ya
Zanzibar ya Vijana chini ya miaka 17 (Karume Boys) kwa ajili ya kushiriki
michuano ya Cecafa ya Vijana nchini Burundi.
Hafla hiyo
imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya Kale kikwajuni
ambapo viongozi mbali mbali walihudhuria wakiwemo wa Wizara ya Vijana Utamaduni
Sanaa na Michezo, baraza la Taifa la michezo na chama cha soka ZFA.
Akitoa nasaha zake
kwa wachezaji na viongozi wa timu hiyo Naibu Lulu amewataka wachezaji hao
kujielewa wao ni nani na jukumu kubwa walilopewa na nchi yao huko wanakokwenda
huku akiwasisitiza kudumisha nidhamu kwani ndio silaha yao.
Amesema kuwa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imewapa jukumu kubwa la kuiwakilisha nchi,
hivyo lazima wafahamu majukumu yao na wanatakiwa kufanya ili kuhakikisha
wanailetea sifa nzuri nchi yao pamoja na kuwa na nidhamu kubwa.
Mapema Katibu Mkuu
wa Wizara ya Vijana Utamaduni Sanaa na Michezo Omar Hassan (King) amezitaja
baadhi ya Taasisi zilizofanikisha safari ya Vijana hao wakiwemo Idara ya
Uhamiaji Zanzibar, Wizara ya Afya pamoja na Hoteli ya Paradise International Hotel
iliyotumika kwaajili ya kukaa Kambi timu hiyo kwa wiki tatu.
Kwa upande wake nahodha
wa timu hiyo Ibrahim Ali Juma (Chafu) amewatoa hofu Wazanzibar na kusema
wategemee Ubingwa kwani kikosi chake anakiamini mno.
Jumla ya msafara wa
watu 29 wakiwemo Wachezaji 23, Makocha 2 na Viongozi 4 wameondoka Zanzibar leo
kwa Ndege kwenda Burundi katika Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi lake April 14 hadi 28, 2018 ambapo Zanzibar imepangwa kundi ‘B’ pamoja na
ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda huku kampeni zake Zanzibar kuwania
kombe hilo zitaanza April 15 kwa kucheza na Sudan katika uwanja wa Gitega
majira ya saa 7:30 za mchana.
Viongozi na Wachezaji wa Karume Boys wakisoma dua baada ya kuagwa |
Kiswandu tueleze kuhusu miaka y'a wachezaji wetu mana nimesikia tumefungiwa napia kulipishwa fain juu ya jambo miaka
ReplyDeleteKiswandu tueleze kuhusu miaka y'a wachezaji wetu mana nimesikia tumefungiwa napia kulipishwa fain juu ya jambo miaka
ReplyDelete