KASSIM KHAMIS WA PRISONS NA ZANZIBAR HEROES KUENDELEA KUUKOSA MSIMU MZIMA BAADA YA KUUMIA KATIKA MCHEZO WA CECAFA WA HEROES NA TZ BARA
Klabu
ya Tanzania Prisons ya Mbeya inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania Bara
itaendelea kukosa huduma ya kiungo mshambuliaji wake Kassim Suleiman Khamis
ambae anaendelea na matibabu ya goti.
Khamis aliiumia goti Disemba 7, 2017 akiitumikia
timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwenye Mashindano ya Cecafa Senior
Chalenj Cup ambapo Heroes waliwafunga ndugu zao Tanzania Bara kwa mabao 2-1, mabao
ambayo amefunga yeye mwenyewe Khamis pamoja na Ibrahim Hamad Hilika, mchezo
uliochezwa katika Uwanja wa Kenyatta Machakos nchini Kenya.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali Khamis aliumia baada
ya kugongana na Daniel Lyanga wa Kilimanjaro Stars na kupelekea kukosa
Mashindano yote ya Cecafa msimu uliopita pamoja na kutoitumikia klabu yake ya
Prisons ya Mbeya.
Akizungumza na Mtandao huu Khamis amesema anaendelea
na matibabu na atokosa mechi zote zilizobakia kwa msimu huu huku akitarajia kujifua
kwaajili ya kujiandaa na msimu ujao wa mwaka 2018-2019.
"Bado goti linanisumbua na sasa naendelea na dozi nilizopewa na Daktari, mazoezi madogo madogo nishaanza lakini daktari kaniambia nikae miezi 2 kisha nianze mazoezi kwaiyo timu yangu ntaikosa msimu wote huu, wakati mwengine najisikia unyonge natamani niwepo na wenzangu nicheze lakini Mungu amepipangia hivi na ndio kheir yangu mana huwezi kujuwa mbele yangu kuna nini". Alisema Khamis.
Katika mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup
yaliyofanyika mwaka jana nchini Kenya ambapo Zanzibar Heroes walishika nafasi
ya pili baada ya kufungwa na wenyeji Kenya kwa penalty 3-2 kufuatia dakika 120
kumalizana kwa sare ya 2-2 ambapo Kassim ndie aliyekuwa kinara wa kufunga mabao
kwa upande wa Zanzibar baada ya kufunga mabao mawili yote akitokea benchi
katika michezo Heroes iliposhinda 3-1 dhidi ya Rwanda na ule wa 2-1 dhidi ya
Tanzania bara.
Comments
Post a Comment