ZANZIBAR YAPANGWA KUNDI LA KIFO PAMOJA NA NDUGU ZAO TANZANIA BARA CECAFA YA VIJANA NCHINI BURUNDI
Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys) imepangwa katika kundi la kifo
kwenye mashindano ya kombe la Chalenji yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018.
Habari
zilizopatikana na Mtandao huu kutoka kwa CECAFA zinaeleza kuwa Zanzibar imepangwa
kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda.
Kwa mujibu wa ratiba
iliyotolewa na baraza hilo inaonesha kuwa Zanzibar itaanza kampeni za
kutwaa taji hilo, kwa kucheza na Sudan April 15 katika uwanja wa Gitega majira
ya saa 7:30 za mchana.
Tayari Zanzibar
imechagua wachezaji 20 na ipo katika maandalizi makali chini ya kocha mkuu Mzee
Ali Abdallah, ambapo Vijana hao wapo kambi katika Hoteli ya Zanzibar Paradise
International iliyopo Uwanja wa Amaan.
Katika Mashindano
hayo yamepangwa makundi mawili yani A ambalo lenye timu za Kenya, Ethiopia,
Somalia na wenyeji Burundi.
Michuano hiyo
inatarajiwa kuanza April 14 katika viwanja vitatu tofauti nchini Burundi vikiwemo
uwanja wa Ngozi, Muyinga na Gitega.
Comments
Post a Comment