ZFA YAITUPIA LAWAMA CECAFA, SASA YAAMUA KUKATA RUFAA


Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) kimepania kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ya kuiondoa timu ya Taifa ya Zanzibar chini ya umri wa miaka 17 (Karume Boys).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Makamu wa Rais wa ZFA Unguja Ali Muhammed Ali amesema kuondoshwa Karume Boys katika Mashindano ya Cecafa ya Vijana yanayoendelea nchini Burundi imesababishwa na Katibu Mkuu wa Cecafa Nicholas Musonye kwa kuwa hakuwasiliana na ZFA kuhusu uchanganuzi wa kanuni inayohusiana na umri wa kucheza kwenye Mashindano hayo.

Amesema wao wapo tayari kufanyiwa uchunguzi wowote juu ya kadhia hiyo huku akizidi kumtupia lawama Musonye kwa kusema anahusika moja kwa moja Zanzibar kuondoshwa kwenye Mashindano hayo.

Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo kanuni ya Mashindano hayo iliwataka wachezaji waliozaliwa kuanzia 01/01/2002 huku Zanzibar ikuwapeleka wachezaji 12 waliozaliwa 2001 jambo ambalo ZFA wamesema hawana taarifa kama wachezaji walotakiwa waliozaliwa 2002 ambapo wao walijuwa walokuwa na umri chini ya miaka 17 hivyo hata walozaliwa 2001 ikiwa bado hawajafika miaka 17 walifikiri wanaruhusiwa ndio mana wakaenda nao ambapo katibu Mkuu wa CECAFA Nicholaus Musonye alisema kuwa ZFA walitumiwa ufafanuzi wa umri kwenye Barua Pepe labda hawazisomi tu.

Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA