KIONGOZI MKUBWA WA ZFA AJIUZULU KUHUSU SAKATA LA KARUME BOYS, KUMBE WALIPOKEA UJUMBE KUTOKA CECAFA


Katibu Mkuu wa chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA) Mohammed Ali Hilali (Tedy) amethibitisha kupokea Barua ya kujiuzulu kwa Makamo wa Rais wa ZFA Unguja Mzee Zam Ali kufuatia sakata la timu ya Taifa ya Zanzibar ya Vijana (Karume Boys) kuodoshwa katika Mashindano ya CECAFA yaliyofanyika nchini Burundi Mwaka huu.

Tedy amesema Mzee Zam ameiwasilisha barua hiyo mapema leo huku akikiri kupokea taarifa kutoka kwa CECAFA inayofafanua kuhusu umri wa Mashindano ambapo amewaomba msamaha kwa kusema alipitikiwa.

Amesema kweli walipokea ufafanuzi wa umri kutoka CECAFA kupitia email ya Mzee Zam na mwenyewe alikiri huku akisema alisahau, hivyo kutokana na kadhia hiyo ameamua kuomba kujiuzulu.

Zanzibar iliondolewa katika Mashindano hayo na kupigwa faini kwa kosa la kuorodhesha wachezaji waliozaliwa kabla ya 01/01/2002 ambapo walikwenda kinyume na kanuni ya Mashindano.

Kutokana na makosa hayo Karume boys imepewa adahabu tatu ikiwemo kuondolewa mashindanoni, inaambatana na faini dola 15,000 (Sh 30 milioni) zinazotakiwa kulipwa na Chama cha Soka la Zanzibar (ZFA), ambapo fedha hizo zitafidia gharama za tiketi, malazi na chakula ya timu katika kipindi chote walichokaa Burundi huku adhabu ya tatu ikiwa kufungiwa kutoshiriki mashindano yanayoendeshwa na CECAFA hadi hapo watakapolipa faini hiyo ambayo inatakiwa kurudishwa FIFA.
Mzee Zam Ali

Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA