KIONGOZI MWENGINE MKUBWA WA ZFA AJIUZULU
Makamo wa Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA
PEMBA) Ali Mohammed nae amejiuzulu rasmi nafasi yake kuongoza chama hicho.
Taarifa kama hiyo ni muendelezo ndani ya chama hicho kufutia
viongozi wengine wajuu akiwemo akiwemo alokuwa Rais Ravia Idarous Faina pamoja
na Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali nao kujiuzulu siku chache zilizopita.
Inaonekana wazi chanzo cha viongozi wote hao kujiweka pembeni
ni kuhusu uzembe uliofanywa kati yao na kupelekea timu ya Taifa ya Zanzibar ya
Vijana U-17 (Karume Boys) kuondolewa katika Mashindano ya CECAFA na kupigwa
faini ya Dola elfu kumi na tano pamoja na kuzuiliwa kutoshiriki Mashindano yote
yatakayoendeshwa na Baraza hilo mpaka kulipa kwa faini hiyo kwa kosa la
kupeleka wachezaji wakubwa waliozaliwa chini ya tarehe 01/01/2002.
ZFA ilizungumza na Vyombo vya Habari kupitia Makamo wake huyo
(Ali Mohammed) na kukataa kuwa CECAFA hawajatuma ufafanuzi wa umri kwa
wachezaji walotakiwa kushiriki mashindano ya CECAFA ya Vijana (U-17)
yalofanyika Burundi mwaka huu huku ikimtupia lawama katibu wa CECAFA Nicholas
Musonye.
Lakini mapema mwezi uliopita alokuwa Makamo wa Urais ZFA
Unguja Mzee Zam Ali alikiri kupokea barua inayofafanua kuhusu umri wa wachezaji
wanaotakiwa kushiriki katika mashindano hayo jambo ambalo likionekana yeye ndio
nambari moja wa kulaumiwa mpaka mwenyewe akaamua kujiuzulu.
flicexFlo-ha Kim Chandler https://wakelet.com/wake/mwPfUkxyFmvoncc5OmkaI
ReplyDeletedielowloudons
bisiab_yu Ruth Gray download
ReplyDeleteclick
click
link
cosnoserna