KOCHA MUU NAE AUTAKA URAIS WA ZFA, IDADI INAZIDI KUONGEZEKA
Kocha wa zamani
wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Wanawake (Zanzibar Queens), Mtende Renger na
Chuoni Mustafa Hassan (Kocha Muu) nae
ametangaza nia ya kugombea Urais wa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar (ZFA).
Amesema kwa vile
analijua vyema soka la Zanzibar na uzoefu wa kuongoza anao ameona ipo haja
kuongoza Chama hicho.
Kocha Muu
atafanya idadi ya Wadau wa soka kuongezeka walotangaza nia ya kugombea nafasi
hiyo baada ya hivi karibuni Mwakilishi wa jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanal,
Abdul Hamid Mshangama na kocha wa Zamani wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar
Heroes) Salum Bausi wote kutangaza nia ya kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi
mdogo unaokuja.
ZFA watalazimika
kufanya uchaguzi kufuatia viongozi wake wakuu kuamua kujiuzulu akiwemo
aliyekuwa Rais Ravia Idarous Faina, Makamo Urais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na
Makamo Urais ZFA Unguja Mzee Zam Ali hivyo nafasi hizo mpaka sasa zipo tupu
huku ikisubiriwa kamati ya Uchaguzi kutangaza tarehe za kuanza harakati za
kufanyika uchaguzi huo.
Comments
Post a Comment