MRAJIS AWAJIA JUU ZFA, KUHUSU KUTAKA VIONGOZI WALIOJIUZULU WAREJESHWE
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mrajis wa Vyama vya
Michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza amesema Ofisi yake inatambua uhalali wa
kujizulu viongozi hao ambao waliandika barua wenyewe.
Juzi wajumbe 13 wa ZFA walikutana Gombani Pemba na kuzikataa
barua za viongozi hao wa juu waliojuzulu huku wajumbe hao wakimtaka Katibu mkuu
wa ZFA kuwaandikia Barua aliyekuwa Rais na Makamo wa Urais ZFA Pemba Ravia
Idarous Faina na Ali Mohammed Ali kurejeshwa kwenye nafasi zao.
Viongozi watatu wakubwa wa ZFA akiwemo aliyekuwa Rais Ravia
Idarous Faina, Makamo Rais ZFA Pemba Ali Mohammed Ali na Makamo Rais ZFA Unguja
Mzee Zam Ali waliandika barua kujiuzulu nafasi zao kuongoza Chama hicho.
Suleiman Pandu Kweleza-Mrajis wa Vyama vya Michezo Zanzibar |
Comments
Post a Comment