TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAAGWA, YAAHIDI KURUDI NA MEDALI ZA DHAHABU
Timu ya taifa ya Riadha ya Zanzibar chini ya miaka 18 itakayoshiriki
mashindano ya riadha ya Vijana ya Afrika Mashariki na Kati yatakayofanyika June
29 na 30, 2018 jijini Dar es salam imeagwa na kukabidhiwa rasmi bendera ya
Taifa ikiwa ni ishara ya kuwakilisha Zanzibar katika mashindano hayo.
Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji 20, viongozi 5 na Waamuzi 10 imeagwa
na Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Lulu Msham
Abdalla katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa uwanja wa Amaan V.I.P na kuhudhuriwa
na Viongozi wa Wizara hiyo na wadau mbalimbali akiwemo Rais wa chama cha Riadha
Zanzibar Abdul hakim Cosmas Chasama na Katibu Mkuu wa chama hicho Suleiman Ame.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Naibu Lulu amesema Wizara yake iko bega
kwa bega na wadau wa michezo huku akiwataka kupambana ili kuchukua ubingwa
ambapo amewasisitiza kudumisha nidhamu kwani ndio silaha muhimu kwao.
Nae Rais wa chama cha riadha Zanzibar Abdul hakim Cosmas Chasama, amesema
kuwa mbali na jitihada kubwa zinazofanywa na chama hicho bado zipo changamoto
nyingi ambazo zinahitaji nguvu za pamoja ili kuhakikisha kuwa riadha inaenda
mbele ambapo amesesema Vijana hao wanatarajiwa kuondoka Zanzibar kesho.
Mashindano hayo yatashirikisha nchi za Kenya, Uganda, Zanzibar, Somalia, Sudan,
Eritrea, Sudan ya kusini, Ethipia, Rwanda, Djibouti na wenyeji Tanzania Bara.
Comments
Post a Comment