TIMU ZA ZANZIBAR ZAANZA VYEMA MASHINDANO YA UMISSETA
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano ya Sanaa na Michezo Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) kwa upande wa Soka Kanda ya Unguja na Kanda ya Pemba zimeanza vyema Mashindano hayo baada ya kupata ushindi katika michezo yao ya kwanza.
Timu ya Kanda ya Pemba wamefanikiwa kuwafunga 1-0 Mabingwa watetezi timu ya Songwe huku bao pekee la Pemba likifungwa na Mohd Said dakika ya 15.
Nao Kanda ya Unguja wamewafunga Mtwara mabao 2-1 kwa mabao ya Said Saleh (Chidi Carrick ) na Talib Ali Issa huku bao pekee la Mtwara likifungwa na Mohd Juma, michezo yote hiyo imechezwa katika Viwanja vya Chuo cha Ualimu hapa Butimba, Mwanza.
Mashindano hayo yataendelea tena leo Jumanne June 5, 2018 hapa hapa Butimba ambapo timu ya Soka ya Kanda ya Pemba watajitupa uwanjani kucheza na Shinyanga mchezo utakaopigwa majira saa 1:30 za asubuhi.
Kwa upande wa Unguja soka watacheza tena kesho Jumatano June 6, 2018 dhidi ya Morogoro.
Michezo mengine ya Mpira wa Kikapu (Basketball) na mpira wa Wavu (Volleyball) kanda ya Pemba watacheza leo majira ya saa 1:30 za asubuhi wote wakiwakabili Shinyanga.

Comments
Post a Comment