UMISSETA ZANZIBAR WAWASILI SALAMA MWANZA, WAPO TAYARI KUBEBA UBINGWA

Msafara wa wanamichezo 170 kutoka Unguja na Pemba wamewasili Mwanza salama, kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Michezo na Sanaa kwa Skuli za Sekondari Tanzania (UMISSETA) ambayo yanatarajia kuanza kesho kwenye viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba.

Akizungumza na Mtandao huu Meneja wa timu ya kanda ya Unguja Abdalla Juma amesema vijana wote kwa ujumla wao Unguja na Pemba wapo katika hali nzuri na hakuna mgonjwa, jambo ambalo ni la kushukuru na wapo tayari kwa ajili ya mashindano hayo.

Nae mratibu wa michezo Kanda ya Pemba Ali Hussein amesema wamejiandaa kutoa upinzani mkali mwaka huu huku akisema Unguja na Pemba wapo kitu kimoja kuhakikisha wanaiwakilisha vyema Zanzibar katika Mashindano hayo.

Kwa upande wao makocha wa michezo mbali mbali kwa pamoja wameshukuru hali ya hewa ya Mwanza ambayo wamesema haina tofauti kubwa na ile ya Zanzibar, jambo ambalo litawasaidia kushiriki vyema michezo hiyo licha ya jua kali lililokuwepo.

Kwa upande wa wachezaji ambao walizungumza na mtandao huu wamesema kuwa wapo tayari kushiriki mashindano hayo na hali ya hewa ya  Mwanza inawaruhusu kushindana, ambapo hivi sasa wanaelekeza akili zao katika mashindano hayo.

Wamesema kuwa licha ya kuwa watashiriki mashindano hayo wakiwa wamefunga, lakini wamesema kuwa si kikwazo ambacho kitawafanya washindwe kufanya  vizuri, kwani hata mwaka jana walishiriki kwenye hali hiyo na walifanya vizuri.

Katika mashindano hayo Zanzibar itaundwa na kanda mbili taofauti ambapo Pemba watakuwa na kanda yao na watashiriki michezo ya Soka,mpira wa Wavu, Riadha na mpira wa Kikapu.
Wakati kanda ya Unguja itakuwa na michezo ya Soka, Riadha, mpira wa Pete,mpira wa Wavu , mpira wa Mikono, mpira wa Meza, Ngonjera na Mashairi.



Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA