ZANZIBAR YAENDELEA KUTESA UMISSETA KWENYE SOKA, MIKONO NA RIADHA
Kikosi cha Mpira wa Mikono Unguja |
TIMU ya kanda ya Unguja mpira wa miguu imeendelea kufanya vyema katika mashindano ya Umisseta, baada ya leo kuwafunga mkoa wa Njombe mabao 2-0.
Mchezo huo ulikuwa mzuri na kupenda kwa muda wote,
Unguja ilianza kupanga mashambulizi ili kutafuta bao la mapema, juhudi ambazo
zilifanikia katika dakika ya 15 kwa bao lililofungwa Ali Hassan.
Baada ya bao hilo kila timu iliendelea kucheza kwa
umakini mkubwa ili kutafuta bao, na juhudi hizo zilizaa matunda kwa upande wa
Unguja, baada ya kufanikiwa kupata bao la pili lililofungwa na Talib Ali dakika
ya 30.
Kwa upande wa mpira wa Wavu bado mambo hayajawa
mazuri baada ya kuendelea kupoteza michezo yake kwa kanda zote Unguja na Pemba.
Katika michezo hiyo kanda ya Pemba ilipoteza mchezo baada ya kufungwa seti 3-0
na Singida, na kanda ya Unguja ilipoteza mchezo dhidi ya Manyara kwa kufungwa
seti 3-2.
Kwa upande wa mchezo wa mpira wa Kikapu kanda ya
Unguja ilitoka na ushindi baada ya
kuwafunga mkoa wa Manyara vikapu 28-22, huku kanda ya Pemba ilikubali kipigo
cha vikapu 40 -28 kutoka mkoa wa Tanga, lakini Unguja lishinda vikapu 62-13
dhidi ya Njombe.
Kanda ya Unguja ilipata ushindi mwengine kwa upande
wa mpira wa mikono baada ya kuifunga
timu ya mkoa wa Manyara mabao 21-7, lakini kwa mpira wa Netiboli Unguja
ilipokea kichapo cha mabao 22-15 kutoka mkoa wa Mtwara.
Michezo ya riadha kanda ya Unguja imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa mbio za mita 100 wanaume na wanawake, mbio fupi za vijiti wanaume na wanawake, hatua ya nusu fainli ya mita 100 itachezwa kesho asubuhi.
Michezo ya riadha kanda ya Unguja imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa mbio za mita 100 wanaume na wanawake, mbio fupi za vijiti wanaume na wanawake, hatua ya nusu fainli ya mita 100 itachezwa kesho asubuhi.
Comments
Post a Comment