ZU YAPAA KWENDA ETHIOPIA KATIKA MASHINDANO YA AFRIKA
Timu ya Soka ya Chuo Kikuu cha Zanzibar University (ZU)
imeondoka Visiwani Zanzibar leo kwenda Makelle nchini Ethiopia kwenye Mashindano
ya tisa ya Vyuo Vikuu vya Afrika (FASU) yanayotarajiwa kuanza rasmi July 1-9,
2018.
Jumla ya msafara wa watu 23, wakiwemo wachezaji 19 na
Viongozi 4 wameondoka saa 3 asubuhi kwa Boti mpaka Dar es salam kisha 12:00 jioni
wakaondoka Dar es salam kwa shirika la Ndege la Ethiopia moja kwa moja mpaka Addis Ababa Mjini Ethiopia.
Akizungumza na Mtandao huu Bandarini Mjini Unguja wakati kikosi hicho
kinaondoka mkuu wa Taaluma wa Chuo hicho Ahmad Majid amesema Chuo chao wamepata
nafasi ya kushiriki Mashindano hayo baada ya kufanya vyema katika Mashindano ya
Vyuo vya Afrika Mashariki na Kati.
Nae Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Mwinyi Ahmad amesema Jumla
ya Vyuo 64 kutoka Nchi mbali mbali za Afrika vitashiriki Mashindano hayo ambapo
kwa Tanzania nzima ZU ndio pekee watashiriki.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa ZU Juma Yussuf Sumbu amewatoa
hofu Wazanzibar huku akisema kikosi chake kipo imara na anaamini watafanya
vizuri.
Wachezaji 19 na viongo 4 waliosafiri ni AHMED ALI SULEIMAN (SALULA), SAID SULEIMAN ALI, ISSA HAMADI MAKAME, YAKOUB OMAR HAMAD, MOHAMED NASSOR MAULID, AWADH OTHAMAN AWADH, SALUM ABDALLAH HAJI, HARITH MAHMOUD KHAMIS, SAID BAKAR SAID, SAID YUSSUF MWINYI, SULEIMAN MIKAIL ANDRIANO, SAID OTHMAN ALI NA MAHAD HASSANI HATIBU.
WENGINE NI NABIL AMOUR JUMA, ALI JUMA MAARIFA, FEREJI SALUM KHAMIS, SULEIMAN ALI NUHU, HABIBU ALI SAID, YUSSUF HAJI RAMADHAN, na viongozi ni MWINYI AHMED MWINYI (MKUU WA MSAFARA), MUHSIN MUSTAFA HASSAN, JUMA YUSSUF KHAMIS (KOCHA) NA BAKAR OMAR BAKAR (DOKTA).
Timu ya ZU ndio mabingwa wa Vyuo Vikuu kwa Tanzania nzima
(TUSA) baada ya mwishoni mwaka jana kubeba taji hilo mjini Dodoma pia ni
mabingwa watetezi wa vyuo vikuu vya Zanzibar (ZAHILFE CUP).
Tuna matumaini ya ushindi. Hakika ss tunawaamini sana juu ya uwezo wenu na matayarisho mliyoyafanya kwa muda mrefu.
ReplyDeleteAllah yu pamoja nass inshaallah