LIGI KUU YA ZANZIBAR KUENDELEA TENA KESHO KAMA KAWAIDA
Mzunguko wa pili wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora inatarajiwa kuanza kesho Jumamosi kwa kuchezwa michezo miwili katika viwanja viwili tofauti. Katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni watacheza kati ya timu ya Mafunzo dhidi ya Zimamoto ambapo muda huo huo katika uwanja wa Gombani kisiwani Pemba Mwenge watakuwa na kazi kucheza na wanajeshi timu ya Hardrock. Katika michezo ya mzunguko wa kwanza Jamhuri walitoka sare ya 0-0 na Mwenge huku JKU nao wakavutana na Zimamoto kwa kwenda sare ya 2-2 ambapo KVZ walianza na ushindi baada ya kuwafunga Mafunzo mabao 2-1 huku Hardrock nao walianza vyema baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Opec.