LIGI KUU ZANZIBAR MSIMU WA MWAKA 2017-2018 KUENDELEA TENA KESHO
Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya nane bora msimu wa mwaka
2017-2018 inatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa kupigwa michezo miwili katika
Viwanja viwili tofauti majira ya saa 10:00 za jioni.
Katika uwanja wa Amaan wataanza kucheza timu ya JKU dhidi ya
Zimamoto ambapo katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba Mwenge wataivaa timu ya
Jamhuri.
Hatua hiyo ndio itakayotoa Bingwa na Makamo Bingwa wa
Zanzibar watakaowakilisha Zanzibar katika Mashindano ya Klabu Bingwa na Kombe
la Shirikisho Barani Afrika ambapo timu nne za Unguja zilizofanikiwa kutinga
hapo ni JKU (Mabingwa Watetezi), Zimamoto (Makamo Bingwa), Mafunzo na KVZ huku
kwa upande wa Kanda ya Pemba ni Jamhuri, Mwenge Opec na Hardrock.
Comments
Post a Comment