KOCHA KING ATANGAZA WACHEZAJI 20 WATAKAOKWENDA ARUSHA ROLLING STONE
Kocha mkuu wa Timu ya Kombaini ya wilaya ya mjini Muhamed
Seif King ametangaza majina ya wachezaji ishirini watakaounda kikosi hicho kinacho
tarajia kuelekea kwenye mashindano ya Rolling Stone Mkoani Arusha Mwezi
huu. Akikitangaza kikosi hicho kinacho husisha wachezaji
wenye umri wa miaka 13 hadi 17 kwa mujibu wa kanuni ya mashindano hayo Kocha King amewatangaza Walinda Mlango Mwinyi Ali, Ahmada Abdulrahman.
wenye umri wa miaka 13 hadi 17 kwa mujibu wa kanuni ya mashindano hayo Kocha King amewatangaza Walinda Mlango Mwinyi Ali, Ahmada Abdulrahman.
Kwa upande wa Walinzi Abdallah Saidi, Abdulahamid Ramadhan, Mudathir Nassor, Mussa Mohamed, Mohamed Haji, Khalid Khamis,Makame Mohamed na Abubakar Suleiman.
Kwa upande wa Viungo wameitwa Yahaya Silima, Fahad Mussa, Kassim Suleiman, Mustapha Muhsin, Yassir Ali, Ibrahim Ali na Mohamed Khamis.
Kwa upande wa washambuliaji ni Ibrahim Yahya , Nassor Saleh, Yussufu Bwanga, Muhamed Daudi na Yussufu Saidi Jussa.
Aidha Kocha Seif King amesema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi
uwanja wa Amani na kinaendelea kujipima mechi za kirafiki na vilabu mbali mbali .
Kombaini ya wilaya mjini itakwenda kwenye mashindano hayo wakiwa ni Bingwa mtetezi baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa huo mara mbili mfulilizo mwaka 2016 na 2017.
Comments
Post a Comment