MKOA WA KASKAZINI UNGUJA KUSHUHUDIA RESI ZA BAISKELI
MASHINDANO ya mbio za baiskeli North Zanzibar Sportive mwaka huu
yatafanyika Agosti 19, Visiwani Zanzibar ambazo zitaanza na kumalizika Nungwi Kazkazini
mwa Kisiwa cha Unguja na zaidi ya washiriki 200 watakimbia Kilometa 50 na 100
kwa wanaume na wanawake.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari
ikuhusiana na matayarisho hayo Mkurugenzi wa Mbio hizo Abrahman
Hussein amesema lengo la kuanzisha mashindano ni kuibua vipaji vya
wakimbiaji wa mbio za Baskeli pamoja na kuisaidia Jamii ambapo wamepanga kusaidia
ujenzi wa Skuli ya Chekechea ya Nungwi.
Amesema mashindano hayo yatasaidia kuongeza idadi ya
Watalii nchini na kuongeza pato la taifa na wananchi mmoja mmoja pamoja na
ongeza la ajira kwa vijana.
Nao baadhi ya Wadhamini wa Mashindano hayo wamesema
wameamua kusaidia Mashindano hayo kwa kumfata Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein ambae analengo la kurejesha vugu vugu
la Michezo Zanzibar.
Kwa upande wake msemaji wa chama cha Baskeli Zanzibar
(CHABAZA) Saleh Kijiba amesema mashindano hayo yamejumuisha wachezaji wa
Zanzibar nzima kwani wapo wengine watakaotoka Kisiwani Pemba kushiriki
Mashindano hayo.
Nao baadhi ya waendeshaji baskeli katika Mashindano
hayo wamesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda huku wakiwashukuru wadhamini
waliojitokeza kudhamini mbio hizo.
Katika Mashindano
hayo ambayo yataanzia Nungwi, watapita Kiwengwa, Pwani Mchangani mpaka Pongwe
kisha kurejea tena Nungwi walipoanzia ambapo washiriki wote watapatiwa zawadi
ya Medali , huku mshindi wa kwanza atapatiwa Shilingi Milioni 1, nafasi ya pili
Laki 5 na watatu Laki 3 kwa Wanaume na Wanawake.
|
Comments
Post a Comment