Posts

Showing posts from May, 2019

JABIR AENGULIWA, HUSSEIN AHMADA AKUBALI YAISHE UCHAGUZI WA ZFF

Image
Mkurugenzi wa Ufundi wa Kamati ya Olympik Tanzania (TOS), Suleiman Mahmoud Jabir, ambae alikuwa anagombea nafasi ya urais kwenye Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) ameondoshwa katika kinyang'anyiro hicho kwa kile kilichoelezwa kukiuka taratibu za uchaguzi kwa kufanya kampeni kabla ya muda. Akizungumza na Kisanduzenj Makamo mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Juma Msafiri Karibona amesema Jabir wamemuondosha kwenye orodha ya wagombea nafasi ya Urais kutokana na kwenda kinyume na masharti yaliyowekwa na kamati inayosimamia uchaguzi huo huku Hussein Ahmad Vuai ambae alikuwa anagombea nafasi ya Makamo wa Urais amejitowa mwenyewe kwenye kinyang'anyiro hicho. ‘’Mgombea Suleiman Mahmoud tumemuondowa kwasababu kakosa sifa kwa vile tumejiridhisha kaanza kufanya kampeni za kimakundi kabla ya muda wa kampeni, na hoja ya pili tumegunduwa   hana maadili mazuri, kwaiyo barua yake tayari tumeshampa na tumemtoa rasmi’’. Tulimtafuta Suleiman Mahmoud baada ya kuondolewa kwenye mc...

HASSAN GHARIB CUP KUANZA JUNE 1

ZOEZI la uchukuaji fomu kwa mashindano ya kombe la Hassan Gharib litaanza Juni mosi mwaka huu. Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha timu 20 yataanza mara baada ya kimalizika kwa funga sita. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mtaribu wa mashindano hayo Talib Haji alisema kuwa fomu zitatolewa kwa timu zozote ambazo zitataka kushiri. Alisema kuwa katika mashindano hayo hakutakuwa na masharti ya timu itakayoshiriki tofauti na mwaka Jana ambapo timu shiriki zilitoka katika jimbo la Dimani pekee. Alisema kuwa timu ambayo itachukuwa fomu italazimika kutoa shilingi elfu tano na kurejesha ni shilingi laki moja kama ndio ada ya mashindano hayo na fomu zitachukuliwa Bweleo Complex. Bingwa wa mashindano hayo ambayo yatakuwa yakifanyika Bweleo atapata shilingi milioni moja na zawadi nyengine. NA MWAJUMA JUMA

MAKOCHA KWENDA KIBAHA KUJIFUNZA MPIRA WA WAVU

JUMLA ya waalimu nane wa mchezo wa mpira wa wavu wanaondoka kesho visiwani Zanzibar kwenda katika Mafunzo ya uwalimu yatakayoanza keshokutwa  mkoa wa Pwani Mkuza Kibaha. Mafunzo hayo ya wiki mbili yanaandaliwa na Shirikisho la dunia la mpira wa wavu (FIBV) yatashirikisha nchi  mbali mbali za Afrika. Kati ya waalimu waliondoka Zanzibar wamo wanawake wawili na wanaume sita huku waalimu wawili wakitokea kisiwani Pemba na yanayodhaminiwa na Kamati ya Olimpic Tanzania TOC . Waalimu hao waliagwa Jana na Uongozi wa Chama Cha Mpira wa Wavu Zanzibar chini ya Mwenyekiti wao Saleh Suleiman. Waalimu hao kwa wanawake ni Hawa Salim Shaibu na Tukekile Mbilinyi na wanaume ni Said Ali Raju, Abdalla Mbarouk Haji, Subeti Pandu Makame, Omar Ali na Masoud Mbarouk Saaduni. NA MWAJUMA JUMA