HASSAN GHARIB CUP KUANZA JUNE 1
ZOEZI la uchukuaji fomu kwa mashindano ya kombe la Hassan Gharib litaanza Juni mosi mwaka huu.
Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha timu 20 yataanza mara baada ya kimalizika kwa funga sita.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mtaribu wa mashindano hayo Talib Haji alisema kuwa fomu zitatolewa kwa timu zozote ambazo zitataka kushiri.
Alisema kuwa katika mashindano hayo hakutakuwa na masharti ya timu itakayoshiriki tofauti na mwaka Jana ambapo timu shiriki zilitoka katika jimbo la Dimani pekee.
Alisema kuwa timu ambayo itachukuwa fomu italazimika kutoa shilingi elfu tano na kurejesha ni shilingi laki moja kama ndio ada ya mashindano hayo na fomu zitachukuliwa Bweleo Complex.
Bingwa wa mashindano hayo ambayo yatakuwa yakifanyika Bweleo atapata shilingi milioni moja na zawadi nyengine.
NA MWAJUMA JUMA
Comments
Post a Comment