MAKOCHA KWENDA KIBAHA KUJIFUNZA MPIRA WA WAVU
JUMLA ya waalimu nane wa mchezo wa mpira wa wavu wanaondoka kesho visiwani Zanzibar kwenda katika Mafunzo ya uwalimu yatakayoanza keshokutwa mkoa wa Pwani Mkuza Kibaha.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yanaandaliwa na Shirikisho la dunia la mpira wa wavu (FIBV) yatashirikisha nchi mbali mbali za Afrika.
Kati ya waalimu waliondoka Zanzibar wamo wanawake wawili na wanaume sita huku waalimu wawili wakitokea kisiwani Pemba na yanayodhaminiwa na Kamati ya Olimpic Tanzania TOC .
Waalimu hao waliagwa Jana na Uongozi wa Chama Cha Mpira wa Wavu Zanzibar chini ya Mwenyekiti wao Saleh Suleiman.
Waalimu hao kwa wanawake ni Hawa Salim Shaibu na Tukekile Mbilinyi na wanaume ni Said Ali Raju, Abdalla Mbarouk Haji, Subeti Pandu Makame, Omar Ali na Masoud Mbarouk Saaduni.
Comments
Post a Comment