JEMBE JENGINE KUTOKA ZANZIBAR RASMI AMETUA YANGA
Timu ya Yanga imemalizana rasmi na Mlinzi
wa timu ya KMC, Ally Hamad Ally 'Kinibu' baada ya kusaini mkataba wa miaka
miwili.
Ally ambae aliwahi kucheza Gulioni FC
ya Zanzibar kabla kwenda Stand United na msimu ulopita akiitumikia KMC.
Kusajiliwa kwa Ally Ally kunaifanya
klabu ya Yanga kuwa na orodha kubwa ya Wachezaji kutokea Visiwani Zanzibar
akiwemo kiungo pendwa Feisal Salum (Fei toto), Mohammed Issa (Moo Banka), Abdul
Aziz Makame (Abui) na wengine wengi ambao wamemaliza mikataba msimu ulopita .
Comments
Post a Comment