MKOA WA KUSINI UNGUJA TISHIO TFF CUP U-17
Kikosi cha Mkoa wa Kusini Unguja |
Timu ya Mkoa wa Kusini Unguja
imeendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kushinda michezo miwili mfululizo ya
mwanzo kufuatia asubuhi ya leo kufanikiwa kuifunga timu ya Mkoa wa Mbeya mabao
2-1 kwenye Mashindano ya TFF ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 (U-17) kwenye
uwanja wa Mabatini Mlandizi.
Katika mchezo huo timu ya Mbeya
ilitangulia kupata bao dakika ya 43 kipindi cha kwanza kwa bao la Bernard Peter
lakini Kusini wakajipanga upya kipindi cha pili kwa kusawazisha na kuongeza bao
kwenye dakika ya 55 na 70 kwa Mabao Ramadhan Mwita Haji na Hafidh Othman Kombo.
Huu ni ushindi wa Pili kwa Mkoa wa
Kusini Unguja kufuatia mchezo wa kwanza kuifunga Lindi bao 1-0 ambapo sasa ina
alama 6 na kuongoza kundi lao B.
Wawakilishi wengine wa Zanzibar
kwenye Mashindano hayo timu ya Mkoa wa Mjini Magharibi leo imejikuta ikipoteza
baada ya kufungwa na Mkoa wa Songwe mabao 2-1 mchezo uliochezwa kwenye uwanja
wa Kibaha.
Comments
Post a Comment