TIMU ZA ZANZIBAR ZIMEAANZA VYEMA MASHINDANO YA UMISSETA
MASHINDANO
ya umoja wa michezo kwa skuli za sekondari Tanzania Umisseta, yameanza kutimia
vumbi katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Ufundi Mkoani Mtwara, huku Zanzibar
ikianza kwa kishindo michezo hiyo.
Katika
Mashindano hayo timu ya mpira wa kikapu ya kanda ya Pemba imetoka na ushindi wa
vikapu 36 -15 dhidi ya Singida huku Unguja nayo mpira wa Kikapu imeanza kwa
kishindo baada ya kuichapa Kigoma vikapu 38-23.
Kwa
upande wa mpira wa Wavu timu ya Kanda ya Pemba imetoka na ushindi wa seti 3-1
dhidi ya Mara kwa wanawake na wanaume Pemba ikakubali kichapo cha seti 3-0
dhidi ya Ruvuma ambapo Unguja Wavu ikachapwa na Mbeya kwa seti 3-1.
Katika Soka
Zanzibar haikuanza vizuri baada ya Unguja kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Dodoma
huku Pemba wakichapwa 3-1 na Katavi ambapo mpira wa Pete Unguja ikifungwa na
Dodoma mabao 21-12.
Comments
Post a Comment