BALOZI SEIF USO KWA USO NA RAIS WA ZFF, WAPEWA USHAURI WA KUKUZA SOKA ZANZIBAR
Seif Kombo Pandu kushoto na Kulia ya Balozi Seif |
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi ameushauri Uongozi Mpya wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} kusimamia
vyema Sheria pamoja na Kanuni ilizojiwekea za kuendesha Mpira wa Miguu ili
kuepuka migogoro inayoweza kuviza viwango vya Soka Nchini.
Akizungumza na Uongozi Mpya wa Shirikisho la Soka
Zanzibar {ZFF} hapo Afisini kwake Vuga, Balozi Seif Ali Iddi amesema vurugu
zilizokuwa zikishuhudiwa kutokea ndani ya Uongozi wa iliyokuwa ZFA kipindi cha
nyuma zilichangia kudorora kwa kiwango cha Soka hapa Nchini.
Balozi Seif amesema Uongozi huo wa sasa unapaswa
kuelewa kwamba wao ndio watakaobeba lawama zitakazotolewa na Wapenzi wa Soka
Nchini endapo kiwango cha Soka kitaonekana kushuka miongoni mwa Wachezaji.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza
Uongozi huo Mpya wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} kwa kuchukuwa madaraka
katika kipindi cha mpito akiwa na matumaini makubwa ya kuimarika kwa mchezo wa
Soka katika kipindi kifupi kijacho Nchini.
Balozi Seif aliuhakikishia Uongozi huo Mpya wa
Shirikisho la Soka Zanzibar kwamba Serikali itakuwa tayari kutoa kila msaada
utaohitajika katika kuona Sekta ya Michezo hasa Mchezo wa Soka unaopendwa zaidi
inaendelea kuimarika kila siku.
Mapema Rais wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF}
Seif Kombo Pandu alisema Shirikisho hilo limejipanga kuendesha Soka
kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za Shirikisho la Soka Duniani {FIFA},Shirikisho
la Soka la Afrika {CAF}na lile la Afrika Mashariki { CECAFA }.
Amesema ni vyema kwa Serikali kupitia Wizara
inayosimamia Sekta ya Michezo kuridhia Mashindano ya Kombe la Mapinduzi
{Mapinduzi Cup}ambayo ndio mashindano makubwa Tanzania yasimamiwe na Shirikisho
hilo.
Ameeleza kwamba hatua hiyo itasaidia sana kuondoa
nadharia ya shughuli za Michezo katika kuendesha Mashindasno hayo kusimamiwa na
Kamati zilizo nje ya Taasisi zinazosimamia Sekta hiyo.
Rais huyo wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} ametoa
wazo katika kuyapa nguvu zaidi Mashindano ya Kombe la Mapinduzi umefika wakati
wa kuandaliwa Timu ya Kombaini inayotokana na Wachezaji wazuri wanaoshiriki
Mashindano ya Ligi za Mitaani za Ndondo Cup kuingizwa katika Mashindano hayo
makubwa.
Seif amesema Ligi za Ndondo Cup hapa Nchini
zimekuwa na mashabiki wengi na kuchukuwa mvuto mkubwa unaopelekea Mji kurindima
wakati wa hatua za Nusu Fainali na Fainali kamili ya Mashindano hayo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Uongozi Mpya wa Shirikisho la Soka Zanzibar {ZFF} uliofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisharasmi. |
MalinMdego Khaled Marte https://wakelet.com/wake/41rMk33lQYwu6sb7IsONj
ReplyDeletekennbeadsmorab
rempbegrampa Jessica Wright Internet Download Manager
ReplyDeleteSpeedify
Yandex browser
workpulinthumb
inefra-ge Paul Hager Software
ReplyDeletereaislugkannrew