WANA JESHI WA ANGOLA KUTUA SAA 7 USIKU KUWAVAA KMKM CAF CL

Wapinzani wa timu ya KMKM kwenye Mashindano ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Afrika Clube Desportivo 1 De Agosto wanatarajiwa kutua Zanzibar saa 7 za usiku (leo kuamkia kesho Jumatano) wakitokea kwao Angola kwaajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza utakaochezwa Agost 10, 2019 saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.

Timu hiyo ambayo ni ya Jeshi la Angola itawasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amaan Karume na kupokelewa na wenyeji wao ambao ni KMKM.

Wawakilishi wengine wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya Malindi wanatarajia pia kuwapokea Wapinzani  wao timu ya Mogadishu City Club (MCC) kutoka Somalia kwaajili ya mchezo wao utakaochezwa Jumapili Agost 11, 2019 kwenye uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni ambapo MCC licha yakucheza ugenini (Amaan) itakuwa ndio mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza baada ya kuliomba Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kucheza michezo yote miwili wa nyumbani na ugenini ichezwe Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

HUYU NDIYE MCHEZAJI MWENYE REKODI YA KUFUNGA MAGOLI MENGI KWENYE MECHI YA TAIFA DHIDI YA BOYS

WACHEZAJI WA 5 WA ZANZIBAR HEROES WAMEITWA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA TAIFA STARS KWAAJILI YA MICHEZO MIWILI YA KIMATAIFA YA KALENDA YA FIFA.

KMKM KUANDAA MASHINDANO YA RIADHA