WASOMALI WANAOCHEZA NA MALINDI CAF WAMEOMBA MECHI ZAO ZOTE KUCHEZWA ZANZIBAR
Wapinzani wa timu ya Malindi ya Zanzibar kwenye Mashindano ya
Kombe la Shirikisho Barani Afrika timu ya Mogadishu City Club (MCC) kutoka
Somalia wameliomba Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) michezo yao yote miwili wa
nyumbani na ugenini ichezwe Zanzibar.
Mchezo huo utachezwa Jumapili Agost 11, 2019 kwenye uwanja wa
Amaan majira ya saa 10:00 za jioni ambapo MCC licha yakucheza ugenini (Amaan)
itakuwa ndio mwenyeji wa mchezo huo wa kwanza.
Katika kujiandaa na mchezo huo dhidi ya Malindi MCC leo
watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya FC Heegan kwenye uwanja wa
Benadir majira ya saa 10:00 za jioni.
Timu hiyo itasafiri kutoka Somalia kwenda Zanzibar Agost 7,
2019 ambapo MCC inawakilisha Somalia kwenye Mashindano hayo baada kuifunga kwa penalty
HorseedSC 4-3 kwenye kombe la Daa (FA CUP) kufuatia kwenda sare ya 0-0 ndani ya
dakika 90 ambapo na Malindi wamepata nafasi hiyo baada ya kuichapa JKU kwa
Penalty 4-3 kufuatia dakika 120 kutoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa fainali wa
kombe la FA.
Timu ya Mogadishu City Club (MCC) imeanzishwa mwaka 1963 kwa
msaada wa Meya wa mji mkuu wa Mogadishu ambapo mbali ya Soka pia inamiliki timu
za michezo mengine kama vile timu ya mpira wa kikapu, Timu ya mpira wa mikono,
Timu ya mpira wa meza, timu ya Lawn tenisi, timu ya mpira wa wavu, Timu ya
kuogelea, timu ya riadha na timu ya Baskeli.
Wawakilishi wengine wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la
Shirikisho Barani Afrika timu ya KMKM watakuwa na kazi kucheza na Deportivo de
Agosto ya Angola mchezo ambao utasukumwa Agost 10, 2019 saa 10:00 za jioni
kwenye uwanja wa Amaan.
Comments
Post a Comment