IBRAHIM JEBA AMEFARIKI DUNIA
Ibrahim Rajab (Jeba) mchezaji wa zamani Mtibwa Sugar na Azam fc amefariki Dunia jioni ya leo Hospitali ya Mnazi Mmoja.
Ibrahim Jeba Mendieta msimu huu alikuwa ameshaanza mazoezi na timu yake ya Chuoni kwaajili ya kutumika tena kwenye ligi kuu Soka ya Zanzibar.
Maziko yatakuwa kesho saa 7 mchana nyumbani kwao Magomeni Mzalendo na kuzikwa Kijijini kwao Ndijani.
Mungu amsamehe makosa yake na amuingize pepon amin.
Comments
Post a Comment