LIGI KUU ZANZIBAR YAANDELEA KWA KISHINDO
Ligi Kuu Soka ya Zanzibar imeendelea tena leo kwa kuchezwa michezo miwili kwenye viwanja viwili tofauti majira ya saa 10 za jioni.
Katika uwanja wa Mao Mlandege wameanza vyema ligi hiyo baada ya kuwafunga Chipukizi mabao 3-1 ambapo mabao ya Mlandege yamefungwa na Yahya Haji (Karoa) akifunga mabao 2 na jengine likifungwa na Khamis Abdallah (Terry) huku bao pekee la Chipukizi likifungwa na Abdallah Mohd.
Na katika uwanja wa Amaan timu ya Maostadh wa Chuoni ikatoka na ushindi wa mabao 3-2 baada ya kuwafunga timu ya Machomane.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumatano kwa kuchezwa mchezo mmoja kati ya Polisi dhidi ya Malindi majira ya saa 10:00 za jioni kwenye uwanja wa Amaan.
Comments
Post a Comment