MALINDI YAANZA VIBAYA NYUMBANI
Wawakilishi wa Zanzibar kwenye Mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika timu ya Malindi wameanza vibaya nyumbani baada ya kukubali kufungwa mabao 4-1 dhidi ya Almasry ya Misri mchezo uliochezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.
Mabao ya Almasry yamefungwa na Mahmoud Wadi dakika ya 27, 39, Hassan Ibrahim dakika ya 32 na Saidou Simpore dakika ya 52 huku bao pekee la Malindi likifungwa na Ibrahim Ali (Imu Mkoko) dakika ya 42.
Mchezo wa marudiano utachezwa Septemba 29, 2019 huko Misri ambapo Malindi anatakiwa kushinda 4-0 ugenini ndipo asonge mbele.
Comments
Post a Comment