ZANZIBAR IMEPANGWA TENA KUNDI MOJA NA TANZANIA BARA CECAFA
Timu ya Taifa ya Vijana ya Zanzibar U-20
imepangwa kundi moja na ndugu zao Tanzania bara kwenye Mashindano ya Vijana ya
Cecafa U-20 inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Septemba 21, 2019 huko
Uganda.
Timu hizo zimepangwa kundi B pamoja
na Kenya na Ethiopia ambapo kundi A wamo wenyeji Uganda, Eritrea, Djibouti na
Sudan huku Burundi ikipangwa kundi C pamoja na Sudan ya Kusini na Somalia.
Baada ya Zanzibar na Tanzania Bara
kupangwa kundi moja Watanzania wengi watayakumbuka Mashindano ya Cecafa Senior
Chalenj Cup mwaka 2017 huko Machakos nchini Kenya ambapo pia walipangwa kundi
moja na Zanzibar ikawachapa Tanzania bara mabao 2-1.
Comments
Post a Comment